Kiswahili Kidato Cha Nne Mada 1 Kuongeza Msamiati Wa Kiswahili

Kiswahili Kidato Cha Nne Mada 1 Kuongeza Msamiati Wa Kiswahili

UUNDAJI

Uundaji wa Maneno

Lugha hukua na kubadilika kila wakati kulingana na maendeleo ya jamii. Kigezo kimojawapo cha kukua na kubadilika kwa lugha ni kuongezeka kwa msamiati. Ili msamiati uongezeke katika lugha sharti maneno mapya yaundwe.

Njia za Uundaji Maneno

Uundaji wa Msamiati hutokea kwa njia mbalimbali zifuatazo:

1. Kubadili mpangilio wa herufi.

2. Kuambatanisha maneno.

3. Kutohoa maneno ya lugha nyingine.

4. Uambishaji wa maneno.

5. Kufanikisha sauti, umbo, mlio na sura.

Kuunda msamiati kwa kubadili mpangilio wa herufi

Neno hujengwa kwa vitamkwa au herufi. Neno jipya lenye maana tofauti huweza kuundwa kwa kubadili mpangilio wa neno linguine

Example 2

Mfano

Neno lima, lina herufi l, i, m, a, herufi hizi huweza kujenga maneno kama mali, kumi,imla, mila.

Neno tua lina herufi t, u, a, herufi hizi zina weza kujenga maneno kama:- tatu, tua, viatu, tatua.

Njia ya kuambatanisha maneno

Kuna njia tatu za kuambatanisha meneno

Njia ya kurudufisha au kukariri neon

Mfano; barabara, sawasawa, polepole, katikati, vilevile.

Njia ya uundaji wa Msamiati kwa kuunganisha maneno mawili tofauti

Nomino na Nomino

Punda + mlia unapata Pundamilia

Bibi + Shamba unapata Bibishamba

Afisa + Elimu unapata Afisaelimu

Mwana + Siasa unapata Mwanasiasa

Bata + maji unapata Batamaji

Kuunganisha kitenzi na Nomino/Jina

Changa + moto changamoto

Chemsha + bongo chemshabongo

Piga + mbizi pigambizi

Zima + moto zimamoto

Kuunganisha maneno mawili na kudondosha baadhi ya herufi

Example 1

Mfano

Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA

Mzaliwa wa mahali Fulani MZAWA

Chama cha Mapinduzi CCM

Nyamamfu NYAMAFU

Kutohoa maneno kutoka lugha nyingine

Kila lugha na tabia ya kuchukua maneno lugha nyingine ili kukidhi mahitaji ya Msamiati. Maneno kutoka lugha nyingine yanapoteuliwa hubadilishwa kimatamshiili ya fuate kanuniza Kiswahili.

Maneno yanayotoholewa kutoka lugha nyingine husanifishwa na asasi za lugha ya Kiswahili ndipo ya ruhusiwe kutumiwa rasmi.

Example 3

Mfano

Neno la Kiswahili Lugha ya Mwanzo Neno Lililotoholewa
Kijerumani Schule
Salama Kiarabu Salaam
Duka Kihindi Dukan
Karoti Kiingereza Carrot
Shati Kiingereza Shirt
Picha Kiingereza Picture
Papai Kihispania Papaya
Meza Kireno Mezi
Shukrani Kiarabu Shukran
Ngeli Kihaya Engeli
Ikulu Kinyamwezi Ikulu
Ng’atuka Kizanaki Ng’atuka
Ndafu Kichaga Ndafu
Namba

Kuunda maneno kwa njia ya uambishaji wa maneno

Hii ni njia ya kubandika viambishi awali na tamati kwe nyekiini. Ujenzi wa maneno hutokana na mzizi mmoja kuonesha maana tofauti ingawa maana zina husiana.

Mfano mzizi: -lim-.Tukipachika viambishi awali na tamati tunapata maneno kama lima, analima, walilima, kilimo, limiana,halitalimwa na ukulima.

Kufananisha sauti, sura au tabia

Example 1

Mfano

Kengele – utokana na sauti ya kengele inapo pigwa

Pikipiki – hutokana na muungurumo wa pikipiki

Ndizi mkono wa tembo – Ndizi inayo fananishwa na mkono wa mnyama tembo

Chubwi – Jiwe au chura atumbukiapo katika kina cha maji.

Mazingira yanayoelezea Kuhitaji Maneno Mapya

Mabadiliko mengi yanatokea kila siku katika nyanja mbalimbali za kimaisha-mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa, kisayansi na kiteknolojia. Katika mazingira kama haya, watu watahitaji kuwasiliana, lugha itahitaji kuunda maneno ili kuwasilisha dhana mpya zilizoibuka. Kwa mfano, maneno kama vile nywila, kisakuzi, udukuzi, puku, talakirishi n.k yameundwa ili kuwasilisha dhana za kiteknoljia kwa Kiswahili.

Undaji wa Maneno katika Miktadha mbalimbali

Mabadiliko ya kimaendeleo yanafanya lugha ihitaji maneno ya kuyafikisha na kutumiwa na jamii. Ili kukidhi mahitaji hayo, maneno mapya yanazuka. Maneno hayo yanaweza kuwa katika fani mbalimbali, kama vile sayansi na teknolojia, siasa, utamaduni na uchumi kulingana na mkondo wa maendeleo. Mfano wa msamiati ni kama vile fedha, ushuru, kumpyuta, ukoloni, hospitali, suruali n.k

Activity 1

Unda maneno katika miktadha mbalimbali

Leave a Comment